MAMBO 7 YA KUZINGATIA UNAPOENDESHA GARI WAKATI WA MVUA AU UKUNGU
Kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwenye makala nyingine kuwa gari ni chombo kinachorahisisha usafiri lakini kinatakiwa kutumiwa kwa umakini na tahadhari kubwa. Umakini na tahadhari zaidi vinahitajika ikiwa utaamua kuendesha gari wakati hali ya hewa ikiwa siyo nzuri, yaani kuna maswala kama vile mvua au ukungu. Taarifa mbalimbali za usalama barabarani zinaeleza kuwa zipo ajali nyingi zinazogharimu maisha na mali za watu ambazo husababishwa na mvua au ukungu. Hivyo ikiwa unataka kuongeza maarifa pamoja na kulinda usalama wako, basi fahamu mambo ya kuzingatia unapoendesha gari wakati wa mvua au ukungu. 1. Punguza mwendo Mwendokasi unaua! Mwendo mkubwa ni hatari sana, lakini ni hatari zaidi mara hali ya hewa inapokuwa mbaya. Kumbuka kuwa wakati wa mvua au ukungu barabara huteleza na ni vigumu kuona njia vyema. Hivyo inashauriwa kupunguza mwendo mara unapoendesha gari wakati wa mvua au ukungu ili uweze kulimudu gari vyema. Pia ukiendesha gari kwa mwendo mdogo utawez...