Posts

Showing posts from June, 2018

MAMBO 7 YA KUZINGATIA UNAPOENDESHA GARI WAKATI WA MVUA AU UKUNGU

Image
Kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwenye makala nyingine kuwa gari ni chombo kinachorahisisha usafiri lakini kinatakiwa kutumiwa kwa umakini na tahadhari kubwa. Umakini na tahadhari zaidi vinahitajika ikiwa utaamua kuendesha gari wakati hali ya hewa ikiwa siyo nzuri, yaani kuna maswala kama vile mvua au ukungu. Taarifa mbalimbali za usalama barabarani zinaeleza kuwa zipo ajali nyingi zinazogharimu maisha na mali za watu ambazo husababishwa na mvua au ukungu. Hivyo ikiwa unataka kuongeza maarifa pamoja na kulinda usalama wako, basi fahamu mambo ya kuzingatia unapoendesha gari wakati wa mvua  au ukungu. 1. Punguza mwendo Mwendokasi unaua! Mwendo mkubwa ni hatari sana, lakini ni hatari zaidi mara hali ya hewa inapokuwa mbaya. Kumbuka kuwa wakati wa mvua au ukungu barabara huteleza na ni vigumu kuona njia vyema. Hivyo inashauriwa kupunguza mwendo mara unapoendesha gari wakati wa mvua au ukungu ili uweze kulimudu gari vyema. Pia ukiendesha gari kwa mwendo mdogo utaweza ku
Image
New song from Naggai ft Linex KITENESI produced by MARQWIZER From SHYTOWN RECORDS CLICK HERE TO DOWNLOAD

NJIA 8 ZA KUOKOA MAFUTA UNAPOENDESHA GARI

Image
Ni wazi kuwa gari linahitaji mafuta ili kusafiri toka sehemu moja hadi nyingine. Lakini swali ni je, unaweza kutawala kiwango cha mafuta kinachotumika? Ndiyo, unawea kutawana kiwango cha mafuta na kupunguza garama za matumizi ya mafuta zisizokuwa na ulazima. Kama unapenda kuokoa kiasi cha mafuta yanayopotea bila sababu ya msingi katika gari lako, basi tumia njia hizi 8 zifuatazo. 1. Kabili upepo Unapoendesha gari upepo hukinzana na gari; hivyo kadri gari linavyokinzana zaidi na upepo ndiyo pia unavyotumia mafuta mengi zaidi. Hivyo basi, usipende kuweka mizigo juu ya gari kwa nje (carrier) au kufungua vioo kwani kutasabisha ukinzani zaidi kati ya gari na upepo. Kwa kukabili upepo vyema utapunguza ukinzani na kuokoa mafuta ambayo yangetumika kukabili ukinzani huo wa upepo. 2. Punguza mwendo Hakuna haja ya kukimbia wakati huna jambo la haraka unaloliwahi; pia hakuna haja ya kukimbia ili uwe mbele ya gari linalofuata. Kufanya hivi kutakupotezea kiasi kikubwa cha mafuta bi

MATUMIZI YA OVERDRIVE KWENYE GARI ZA AUTOMATIC

Image
Overdrive ni nini? Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.   Over drive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo mana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katka gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi rpm inaweza kua 4000rpm. Katka barabara tambarare. ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara tambarare. Utajuaje kuwa Overdrive ipo On au Off? Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako inamaanisha kuwa Overdrive ipo off na pindi Ki