Posts

Showing posts from May, 2018

WHEEL AND TYRE

Image
Wheel ni nini ? Huu ni muunganiko (combination) wa tire pamoja na rim.  Katika saizi mbalimbali zitokanazo na ukubwa na aina ya gari. (Size hizi zinaendana na radias- kipenyo cha kati)           Tyre ni nini?  Hii ni raba pana yenye umbo la duara ambayo inawekwa juu ya rim kwa kawaida raba hii inapoambatanishwa pamoja na rim tunapata kitu kimoja amabacho ni wheel (gurudumu) Rim ni nini? Hiki ni kifaa chenye umbo la mduaraambacho kimeundwa eidha kwa alminiumalloy au chuma (cast iron).             Faida na kazi za wheel (gurudumu ) Inafanikisha mwendo katika chombo husika, baada ya kukamilisha mzunguko wa gurudumu. Hii inajieleza  yenyewe haihitaji uwe umeenda chuo cha VETA, fikiria kwamba unainjini yako , gear box , propeller, sheft, diferential alafu hauna magudumu je? Gari itajiongea kwenda uwelekeo wowote? Jibu ni hapana, hivyo gurudumu ni muhimu sana. Inabeba mzigo wote uliopo katika gari Hapa tuelewe ya kwamba mzigo si mpaka uweke mafenesi na maaembe katika g

LUBRICATION SYSTEM (MFUMO WA ULAINISHAJI)

Image
LUBRICATION SYSTEM (MFUMO WA ULAINISHAJI) Huu ni mfumo miongoni mwa mifumo mingi inayopatikana katika gari. Huu ni mfumo muhimu sana kwasababu ni mfumo ambao unakinga injini kwa kuzuia msuguano wa sehemu mbili zinzzozunguka hususani chuma na chuma Mfumo huu wa ulainishaji unaruhusu chombo kufanya kazi kwa wepesi (smooth operation) lakini si hivyo tu bali pia mfumo huu unakifanya chombo kuwa na maisha marefu (maintain span of life) Bila mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kunaweza kupelekea Kusizi kwa injini kutokana na ukavuwa ndanu ya injini hivyo kupelekea joto la injini kuongezeka na hatimae kushindwa kabisa kufanya kazi. Sahau utakavyo jisahau lakini usisahau kujua kupatikana kwa oili katika gari wakati wote kabla ya kutumia gari lako kwa kiwango kinachopaswa kuwepo wakati wote. Mfumo huu ni kitovu cha usalama wa gari lako hivyo iwapo haujatumia nguvu ya kufanya umuhimu wa kuweka oil kwa wakati utahatarisha gari lako AINA ZA MFUMO HUU WA ULAINISHAJI Mist Lubrication Hi

MFUMO WA BREKI YA GARI

Image
Huu ni mfum o miongoni mwa mifumo mbalimbali inayopatikana katika gari, Mfumo huu ni katika mifumo muhimu kiusalama katika gari KAZI YA MFUMO WA BREKI Mfumo wa breki hufanya kazi zifuatazo, Kupunguza mwendo Kusimamisha mwendo AINA ZA BREKI Kuna aina mbili za breki kama ifuatavyo Mechanical Break Hydraulic Break Air Brake MECHANICAL BRAKE Hii ni aina ya breki ya kimakenikali ambayo inayegemea nguvu ya dereva tu katika utendaji kazi wake Aina hii ya breki imekuwa ikitumika katika magari ya zamani lakini kwa sasa si rasmi Picha ya mfumo huu ni kama unavyoona breki ya baiskeli. Kama hauna baisikeli nenda kaangalie hata baisikeli ya jirani ili ujue breki za mekamikali zinavyofanya kazi katika mfumo wake VITU VINAVYOJUMLISHWA KATIKA MFUMO HUU Pedali (Brake pedal) Hiki ni kifaa kinachotumiwa na dereva kuvuta breki na kupsimamisha au kupunguza mwendo wa gari kwa wakati anapopaswa kufanya hivyo. Springi Mrejesho (Return Spring) Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kusaid