LUBRICATION SYSTEM (MFUMO WA ULAINISHAJI)

LUBRICATION SYSTEM (MFUMO WA ULAINISHAJI)
Huu ni mfumo miongoni mwa mifumo mingi inayopatikana katika gari. Huu ni mfumo muhimu sana kwasababu ni mfumo ambao unakinga injini kwa kuzuia msuguano wa sehemu mbili zinzzozunguka hususani chuma na chuma
Mfumo huu wa ulainishaji unaruhusu chombo kufanya kazi kwa wepesi (smooth operation) lakini si hivyo tu bali pia mfumo huu unakifanya chombo kuwa na maisha marefu (maintain span of life)
Bila mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kunaweza kupelekea Kusizi kwa injini kutokana na ukavuwa ndanu ya injini hivyo kupelekea joto la injini kuongezeka na hatimae kushindwa kabisa kufanya kazi.
Sahau utakavyo jisahau lakini usisahau kujua kupatikana kwa oili katika gari wakati wote kabla ya kutumia gari lako kwa kiwango kinachopaswa kuwepo wakati wote.
Mfumo huu ni kitovu cha usalama wa gari lako hivyo iwapo haujatumia nguvu ya kufanya umuhimu wa kuweka oil kwa wakati utahatarisha gari lako
AINA ZA MFUMO HUU WA ULAINISHAJI
Mist Lubrication
Hii ni aina ya mfumo wa ulainishaji ambao unataumia kiasi kidogo sana kwa kawaida ni asilimia mbili au tatu ya oili ndio hutumika katika mfumo huu
Utendaji kazi wake
Kiasi kidogo cha oili kisichozidi asilimia tatu kinachanganywa namafuta kwa kawaida mafuta hayo huwa ni gasoline (petrol) baada ya mafuta hayo yanapelekwa moja kwa moja kwenye carburetor hapo mafuta yatachanganyika na upepo (hewa) na kubadilika kuwa katika mfumo wa gesi papo yatasafirishwa moja kwa moja mpaka chumba cha muwako (COMBUSION CHAMBER) kwaajili ya kutimiza mapigo ya injini, wakati huo oili itakuwa imehifadhiwa kuzunguka crank case katika mfumo wa ukungu na kudondosha matone ya oili na matone  hayo yatalainisha ukuta w silinda (cylinder wall) crankshaft na bearing zote pamoja camshaft
Aina hii ya ulainishi hutumika hasa katika injini za two stroke (mapigo mawili) kwa mfumo katika injini za baadhi ya pikipiki na majenereta WET SUMP LUBRICATION
Splash Wet sump lubrication
Hii ni aina ya ulainishaji ambayo inahusisha oili sumjp au oili pan katika eneo la chini kabisa ya injini ambayo ianahifadhi oilo ndani yake ambayo inatumika kulainisha camshaft,crankshaft,bearing,cylinder wall na sehemu zote zinazohitajika kulainishwa kwa kutumia oil.
Aina ya Wet sump lubrication
  1.  Splash wet sump lubrication
Hii ni aina ya ulainishaji ambayo inatumika hasa katika injini ndogo za mapigo manne zisizojongea (small stationary four stroke engine)
Katika aina hii oili inachapwa kwa kutumia mfuniko wa kipande unganishi na ile ya bearing (cup of comnnecting rod and bearing) kupitia vikombe vilivyo katika mifuko hiy kwa hiyo baada ta oili kuchapwa itasafiri kwa nguvu kubwa mpaka katika crank shaft bearing,connecting rod,cylinder wall na cam shaft
  1. Splash and pressure wet sump lubrication
Hii ni aina ya ulainishaji ambayo inatumia kuchapa oili na wakati huo huo inatumia pampu kusafirisha oili kwa mgandamizo (pressure)
Aina hii ya ulainishaji kwa kawaida hutumika katika ijini za kati na zile kubwa zinazjongea na zile zisizo jongea (small nad huhe movable and stationary engine)
Katika mfumo migIfuniko ya bearing na connecting rod itakuwa ikichapa oili kuipeleka katika sehemu zinazoitaji oili lakini pia wakati huo huo oili  inasukumwa kwa mganamizo kwa kutumia pampu ili kulainisha bearing,connection rod,cylinder wall, camshaft na kila sehemu inayopasa kulainiswa kwa oili
Mfumo huu umehusisha njia hizo mbili yani splash na pressure kwa sababu hizi njini ni kubwa hivyo splash kutokana na muundo wake haiwezo kukidhisehemu kubwa hivyo ikaongezwa pampu ili kufanikisha ulainishaji katika sehemu zote zinazohitaji kulainishwa
Presurized wet sump lubrication
Hi ni aina ya ulainishaji ambayo inatumia mgandamizo wa pampu pekee kukidhi ulainishaji
Mfumo huu hajachagua aiana ya injini hivyo unatumika katika injini ndogo, za kati na zile kubwa. Aina hii ndio aiana pekee ambayo imelkubalika na wahandisi wengi wa maswala uya uundaji wa injini (engine creation) Kutokana na kutenda kazi vema Zaidi
Aina hii ni aina ambayo inatumika katika injini ambazo zinazobeba mizigo mizito na zile zenye spidi kubwa na ndio maan tumeona mfumo huu kutumiaka Zaidi katika magari na vyombo vinginevyo vya usafiri.
Dry-Sump Lubrication
Hii ni aina ya mfumo wa ulainishaji ambao tenkil lake lipo nnje ya injini
Katika mfumo huu wa injini yake haihusishi tanki l oili ndani yake hivyo badala yake tanki lipo nnje ya injini na inafanya kazi kwa kutumia pampu kusukuma oili kwa mgandamizo kupitia oili filter kwenda kwenye matumizi kupitia katika oili cooler (kipooza oili)
Vitu vinavyohusiswa katika mfumo wa ulainishaji
  1. Oil pan (oil sump)
Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kuhifadhi oili kabla na baada ya amatumizi
Hiki kifaa ndio tanki tegemewa katika uhifadhi wa oili hasa katika aiana ya ulainisha ji wa wet sump na ile ya dry ingawa katika hii lipo nnje ya injini
  1. Oil trainer
Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kuchuja oili. Hili ni chujio la awali (primary) ambalo linatumika kuchuja uchafu mkubwa uliopo katika oili
  1. Oil pump
Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kusukuma oili kwa mgandamizo (pressure) kwenda katika matumizi yaani ulainishaji wa sehemu mbalimbali za injini ambazo zipo katika msuguano
  1.  Oil line
Hizi njia za oli ambazo zipo katika brock la injini pamoja na cylinda head
Hizi njia zipo kwa ajili ya kuruhusu oil kufika katika zile sehemu tu ambazo oil inahitajika na haitoweza fika na ikifika ni tatizo mfano wa sehemu ambazo oil haipaswi kufuka ndi nadani ya chumba cha muwako combustion chamber
  1. Oil garaly
Hiki ni kifaa mabacho kinatumika kutupa oili katika kuta za silinda ()cylinder wall) ambapo pana msuguano wa hiyo kuta na piston na joto kubwa huzalishwa katika eneo hili hadi kufikia kiasi cha 1800 sentigredi mpaka 8000 sentigredi
  1. Oil cooler
Hiki ni kidfaa ambacho kinatumika kupooza oil baada ya kupita katika matumizi, ikiwa oil imepita katika sehemu zenye joto kubwa kama tulivyoona ktika namba tano hapo juu yahitajika kupoozwa hivyo itapoozwa katika oil cooler
  1. Oil filter
Hiki ni kifaa mabacho kinatumika kuchuja uchafu mn=dogo mdogo kabls oili hsijsfika katika matuzizi. Hiki ni kifaamuhimu katika usalama wa mfumo huu na nilazima kubadilisha oili filter kila unapo badilisha oili kwanji usipoibadilisha ni sawa sawa na haujabadilisha oili bali umeiavha ile ile japokuwa umebadilisha kwa kuwa uchafu utakuwa umejaa katika filyer na kulazimisha kubadili uhalisia wa oili kwani nayo itachafuliwa
Kazi ya oili katika injini
Oil kimsingi inakazi kuu mbili katika injini ambazo ni:-
  1. Kulainisha sehemu zote zenye msuguano katika injini kama vile crank shaft na bearibg au cam rob na sehemu nyinginezo.
Faida na kazi za oili tajwa hapo juu
  1. Kuhakikisha maisha marefu ya injini
Unapofanyika ulainishaji ulio sahihi na wenye kufuata utaratibu maisha ya injini yanaongezeka kwa sababu sehemu zote za mzunguko zitakuwa zinafanya kazi kwa ulaini hivyo hapatatokea kusagika kwa sehemu hizo, hivyo injini yako itakuwa bado inauhakika wa kuishi miaka mingi baadaye.
ii. Engine kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kasi yoyote ilenitakayo kuendana na uwezo wake kwasababu sehemu zote za mgusanozinazozunguka, zinazunguka kwa nguvu ndogo lakini mzunguko wake unakuwa mkubwa zaidi ya nguvu iliyotumika kutokana na ule ulaini tofauti na engine ambayo haihudumiwi vizuri katika masuala ya service.
  1. Kupooza injini
Kazi ya pili ya oil katika injini ni kupooza injini.
Kipindi oil inafanya kazi yake kulainisha sehemu zinazosuguana pia inaondosha kiasi cha joto kwa kawaida ni joto la asilimia saba katika joto lote la injini hivyo kuna uwezekano mkubwa wa injini kuwa na joto kupita kiasi (cover heat) endapo oil haipo katika kiwango sahihi au isipokuwepo kabisa.

Kwa niaba ya #Evolution na #Team Cruiser, asante. 
Kwa maoni na ushauri acha comment yako hapo chini. 

Comments

Popular posts from this blog

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

UMEME WA MAGARI

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI