Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)
Gari ni chombo ambacho kinahusisha mifumo mbalimbali muhimu katika ufanikishaji wa kazi yake. Ni kama vile binadamu alivyo na mifumo katika mwili wake kwamfanokwabinadamukuna mifumo mingi kama vile Mfumo wa chakula, Mfumo wa damu, na mfumo wa utoaji taka mwilini. Hivyo kwa kuanza kuchambua mifumo mbali mbali kati gari, leo tuanze kuchambuamfumo wa upoozaji, kwa kiingereza unaitwa cooling system.
Mfumo wa upoozaji ni mfumo muhimu sana katika gari kwasababuutendaji kazi wa injini katika hiyo gari unazalisha joto kila inapofanya kazi, hivyo yahitaji kupoozwa kwa wakati kuepusha madhara.
Aina za mifumo ya upoozaji wa injini katika gari
– Kuna aina mbili za upoozaji wa injini katika gari kama ifuatavyo:
Upoozaji wa maji (water cooling system)
Hii ni aina ya upoozaji wa injini kwa kutumia vifaa mbalimbali vinavyohusishwa katika mfumo wa upoozaji unaotumia maji. Katika mfumo huu umeundwa na vifaa vifuatavyo.
REJETA
Hiki ni kifaa muhimu katika mfumo wa upoozaji injini wa maji kinachotumika kupoozea maji. Hiki ni kifaa kilichokusanya sehemu tofautitofauti katika umbile lake, kwanza kabisa kunatanki la juu ( upper tank) tanki la chini (Lower tank) mifuniko (Radiator cap) mirija ya kusafirisha maji toka tanki la juu kwenda tanki la chini (Radiator cube) Pia kuna njia za wazi za kusafirishia joto ( Radiator Fins)
PAMPU YA MAJI
Hiki ni kifaa muhimu pia katika mfumo huu kwa sababu kinafanya kazi ya usukumaji maji kwa mgandamizo (pressure) ili kuyafanya maji yawe katika mzunguko mzuri (good circulation) ili kupooza injini kwa wakati sahihi (right time)
FENI (RADIATOR FAN)
Hii feni ya rejeta inatumika kuisaidia rejeta kupoza maji kwa kutumia hewa ambayo inasafiri na joto lililopo katika maji. Kuna aina mbili za feni kuna feni ya inayowaka muda wote( all time) ambayo ni ( manual operated) hii inazungushwa na mkanda (fan belt) na feni inayowaka kwa muda mfupi (short time) ambayo ni inajiendesha yenyewe (automatic operated.) na hii huendeshwa na umeme zaidi.( na hutumika zaidi kwa gari za kisasa)
THEMOSTAT VALVE
Hii ni valve ambayo inatumika kuhisi joto nakutunzajoto la injini. Tunasema inahisi joto kwa sababu kiuhalisia ikifikwa na joto kuanzia asilimia 88 na kuendelea inapata taarifa ( kwakuhisi) hivyo hufunguka na kuruhusu maji yenye joto hilo kutoka kwenye injini na kuruhusu maji yaliyopoozwa katika rejeta kuingia katika injini. Lakini pia tunasema inatunza joto kwasababu pindi gari lizimwapo themostart inafunguka katika kiwango cha joto la asilimia 87 . kushuka chini hivyo itakuwa imetenganisha maji yaliyopo kwenye injini na yale yaliyopo kwenye rejeta hivyo maji yaliyopo kwenye injini yatasalia yakiwa na joto hivyo yatasaidia gari kuwaka kwa haraka bila shida hususani kwenye miji yenyebaridi kama vile Kilimanjaro, mbeya na kwingineko.
HORSE PIPE
Hili ni bomba ambalo husafirisha maji kutoka kwenye injini kwenda kwenye rejeta.
UPOOZAJI WA HEWA (AIR COOLING SYSTEM)
Hii ni aina ya pili ya mfumo wa upoozaji wa hewa si mfumo rasmi sana kwa sasa mfumo huu umetumika sana zamani hususani katika maeneo ya ukanda wa majangwa kama vile jangwa la sahara.
Katika mfumo huu gari linapoozwa naupepo tu, kupitia mianya huru ya kusafirishia joto (fins)
MATATIZO KATIKA MFUMO WA UPOOZAJI
Mara nyingi tatizo kubwa lililopo katika mfumo wa upoozaji ni joto kupita kiasi (over heat)
Joto kupita kiasi ni kile kitendo ambacho injini inaongeza joto lake kufikia kuathiri utendaji kazi wake wa kawaida.
SABABU ZINAZOCHOCHEA JOTO KIPITA KIASI KATIKA INJINI (OVER HEAT)
Yafuatayo ni mambo yanayo sababisha injini kuwa na joto kupita kiasi
Kuharibika kwa pump ya maji (Defective water pump)
Hii inachangia injini kuwa na moto kupita kiasi kwa sababu maji yana kuwa tuli (yanatuama) hivyo ni ngumu kupozwa badala yake huongeza joto kwani maji yaliyopo kwenye injini yatakaa huko ya kiongezeka joto na hatimae hata yaliyopo kwenye rejeta yatapata joto pia hivyo lazima patatokea upatikanaji mkubwa wa joto katika injini.( engine over heat.)
Kukatika kwa mkanda wa feni (fan belt broken)
Endapo mkanda wa feni umekatika yani( fen belt broken) lazima engine ita over heat kwa sababu upoozwaji wa maji katika rejeta hautofanyika kwani feni inasaidia rejeta kupooza maji hivyo engine over heat itatokea.
Kuungua kwa cylinder head gasket (Gasket wear)
Iwapo engine cylinder head gasket imeharibika lazima mfumo wa upoozaji utaathirika kwa sababu italeta muingiliano wamaji na hewa iliyo ndani ya cylinder (chemical) correction mixture na muingiliano kati ya maji na oili kwahiyo lazima gari litakuwa na joto kupitakiasi.
Kuharibika kwa themostart valve (wear of thermostat valve)
Endapo themostat valve imeharibika haitoruhusu maji kuzunguka badala yake kuwa tuli (kutuama) hivyo maji yatakuwa na joto kupita kiasi kwa hivyo injini itakuwa na joto kupita kiasi.
Kuvuja kwamaji (Water LEAKAGE)
Ikiwa maji yanavuja katika mfumo wa njia yoyote ile kwamfano ikiwa rejeta imetoboka au bomba (pipe) imetoboka au sehemu yoyote ile inayopita majina haikufungwa kikamilifu kwa kawaida rejeta haitakiwi kuwa na maji machache bali inahitajika kuwa imejaa muda wote wa kazi zake
Upepo katika mfumo
Endapo mfumo umeingiwa na hewa injini itachemsha kwa sababu maji yatagawanywa katika vipande vipande hivyo hayatakuwa katika mtiririko wake uliosa hihi, hivyo husababisha ugumu katika kuyapoza na kupelekea injini kuchemsha.
MADHARA YANAYOTOKANA NA JOTO KUPITA KIASI KATIKA INJINI
Kwanza ni kuungua kwa cylinder head gasket iwapo injini inapata joto kupita kiasi itapelekea gasket ya cylinder head kuungua hivyo italeta matatizo mengine Zaidi kama vile kuchanganyika kwa oil na maji lakini pia kupotea kwa mgandamizoGari kukosa nguvu
Hii ni baadaya cylinder head gasket kuunguwa pigo la compression inakuwa dhaifu kutokana na kupotea kwa kiasi cha hewa au mchanganyiko na hewa. Hakikisha mkanda wako wa feni ukosawa au feni yako imefungwa kwa wakati (automatic fan)
ANGALIZO
Pindi utakapoona taa au gauge inayoashiria joto kupitakiasi(over heat) paki gari lako pembeni kuepusha matatizo zaidi katika gari lako.
nilikuwa nauliza dempa linaweza kusababisha gari ichemshe
ReplyDeletenimeshA Anza kuelewa
ReplyDeleteGood explanation
ReplyDeleteLand cruiser yangu nilitembelea km 20 Nika Kuta oil ndani ya rejeta tatizo ni nini
ReplyDeleteKama mtaalam alivyoelezea hapo juu inawezekana ni cylinder head gasket gari inapata joto kupita kiasi na kupelekea cylinder head gasket kuungua
ReplyDeleteHaha
ReplyDeleteYaani nimeanza pata mwanga sasa.nilikuwa naichukia gari
ReplyDeleteAsante kwakunielimisha mbalikiwe sana
ReplyDeleteMaelezo mazuri sana
ReplyDeleteMKUU NINGEPENDA UBADILISHE MUONEKANO WA BLOGU YAKO PIA NINAWEZA FANYA KAZI IYO KUWA KAMA YANGU
ReplyDeletewww.safariafricablog.com
Inaaeleweka mkuu
ReplyDeleteGari langu nkiliwasha huwa taa ya ABS haizimi hapo mkuu tatizo litakuw nn??
ReplyDelete