Posts

Showing posts from August, 2018

PROGRAM UNAZOPASWA KUWA NAZO KWENYE COMPUTER

Image
Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu hatokuja kuweza kuyafanya kirahisi. Lakini, haiwezi kufanya kitu bila kupewa amri Fulani. Zaidi haiwezi kujitunza, inakutegemea wewe kwa kila kitu. Computer yako ni muhimu sana, zipo sababu nyingi za kuunga hilo mkono, umenunua kwa bei ghali (..Hata kama umenunua Used..). Programu sio pekee ni muhimu lakini ni vyema zaidi kuwa nazo kama kweli unaijali computer yako. Kabla hata ya kwenda mbali, Tembelea  Ninite  , hapa utaweza kudownload program zote za muhimu bure ingawa baadhi ni kwa ajili ya kujaribu kwa muda tu na baadae itabidi ununue, usiwaze achana na zile zinazohitaji ununue zipo program nyingi sana tu za bure na bora zaidi. Tia maanani aina ya computer yako ili pindi unapo download software iweze kufanya kazi. Hapa naongelea aina kama ni 32-Bit au 64-Bit. Computer zinaweza kuwa kuwa na Operating System moja kwa mfano Windows 7, kampuni moja kwa mfano Samsung au Dell, lakini zina uwezo wa Bit tofauti, program ya 64-

MAMBO 10 YAKUZINGATIA KABLA NA WAKATI WA KUENDESHA GARI UMBALI MREFU.

Image
Kuendesha gari ni suala linalohitaji umakini na utulivu mkubwa, hasa pale unapoendesha gari umbali mrefu. Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri. Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na wakati wa kuendesha gari umbali mrefu. 1. Kagua na andaa gari Kabla ya safari yoyote gari linahitaji kukaguliwa na kuandaliwa, hasa kabla ya safari ndefu. Kuna mambo kadhaa unayohitaji kuyakagua kwenye gari lako: Kagua hali na ubora wa magurudumu. Hakikisha magurudumu yamejaa vizuri na hayajazeeka. Kagua mafuta lainishi (oil). Hakikisha gari yako ina mafuta lainishi ya kutosha tena ya ubora unaotakiwa. Kagua kiasi cha maji. Maji? Ndiyo maji ni muhimu sana kwenye gari kwa ajili ya kupooza injini ya gari pamoja na kusafishia vioo. Kagua utendajikazi wa injini. Hakikisha injini yako inafanya kazi vizuri