JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI
SEASON 2
LIJUE GARI LAKO.
Mfumo wagea Gea za Gari za aina mbali mbalizenye kutumia mfumo wa Manyo ( Manual)
CLUTCH ; Kazi yake ni kuondoa gari na kutenganisha Engine na Gearbox.
BRAKE ; Kazi yake ni kupunguza mwendo na kusimamisha gari
ACCELERATOR; Kazi yake ni kuongeza mwendo kasi wa gari na muungurumo na inapoachiwa kidogo mwendo hupungua, inaongeza kasi ya uhcomwaji wa mafuta.
Ni Muhimu Kukumbuka kuwa Unapotaka kusimama unatakiwaq kukanyaga Clutch na Brake kwa pamoja ili gari lisizime linaposimama.
Kazi ya gea namba moja Ni kuondoa gari na kupanda mlima mkali na wakati wa kuteremka mlima mkali
Kazi ya gea namba mbili Ni kuifanya gari kuwa nyepesi zaidi na kuongeza mwendo
Kazi ya gea namba tatu na nne Ni kufanya gari kuendelea kuwa jepesi zaidi na kuongeza mwendo
Namna ya kupanga gea kutoka gea nzito kwenda gea nyepesi;
Kutoka 0-10 MPH Gea . No 1
Kutoka 10-20 MPH. Gea . No 2
Kutoka 20-30 MPH. Gea. No 3
Kutoka 30-40 MPH. Gea. No 4
Kutoka 40-50 MPH Gea. No 5
Kutoka 50-120 MPH. Mwendo utaendelea kuzaliswa na gia No 1 & 2
Jinsi ya kupangua gea kubwa kwenda gia ndogo
Kama gari lilikuwa linatembea kiasi cha mwendo upatao 60MPh itakubidi upunguze mwendo hadi 50MPH au 40MPh ndipo uingize gia nambari nne
Endapo inatembea mwendo kiasi 40 MPH itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 30MPH ndipo uingize gia nambari tatu
Kama gari ilikuwa inatembea kiasi cha mwendo upatao 30MPH itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 20MPH ndipo uingize gea nambari mbili
Dash board ni chombo ambacho kinamjulisha na kumwezesha dereva kugundua hitilafu zinazoweza kujitokeza anapoendesha gari barabarani kwa mfano
· Kusoma speedmeter – hiki ni chombo ambacho hupima kasi au mwendo wa gari
· Mail gauge – hiki ni chomboambacho hupima au kuhesabu au kurekodi ni mwendo au umbali gani gari limetembea
· Fuel gauge – ni kipimo cha kuonyesha ni kiasi gani cha mafuta aidha Petrol au diesel iliyoko kwenye tank la gari
· Oil gauge – ni kipimo chenye kufanya kazi ya kuonyesha ni kiasi gani cha oil kimebakia kwenye injini
· Water temperature gauge ni kipimo ambacho kinaonyesha joto la injini limepanda kiasi gani na pia kuonyesha maji yamepata moto kiasi ghani kwenye radiator
· Alternator gauge au alternator charge hiki ni chombo cha kuonyesha kuwa kifua umeme katika gari hakifanyi kazi kwa msingi huo maana yake ni kuwa haichaji na hivyo maana yake ni kuwa umeme haufuliwi
· Right indicator – ni taa maalumu yenye mlio Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda upande wa kulia
· Left indicator – ni taa maalumu yenye mlio Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda kushoto
Dash Board kama inavyoonekana katika mchoro chini.
Katika Dash Board kunakuwa na maswala kadhaa yanayoweza kusoma mambo kadhaa yafuatayo
0 2 6 8 6 4 2
|
Water temp
|
Brake Light
|
Alternator
|
Fuel gauge
|
Right
|
Left indicator
|
Fuel
|
UTUNZAJI WA GARI
Katika utunzaji wa gari kwa ujumla tunazungumzia ukaguzi wa gari.Ukitaka gari lako liwe katika hali nzuri kila ulitumiapo/kuwa na uhakika wa usalama wako na wa gari lako liwapo barabarani, ni muhimu sana kulikagua hari kila siku asubuhi kabala ya kuliendesha na pia kuwa na utaratibu wa kulifanyia service kila linapotembea kilomita kadhaa.
Ukaguzi wa gari
1. Kitu cha kwanza kabisa ni kulikagua gari lako kwa nje, utafanya ukagfuzi wa matairi kwa kuangalia
· Upepo na nati kama zimelegea au la
· Kashata za Matairi kama hazijaisha yaani ziko kipara
Kisha utafungua Bonet na hapa utaangalia
· Maji kwenye rejeta (radiator) kama yapo
· Oil kwenye injini kwa kutumia deep stick
- Hakikisha unapopima oil gari liko katika tambarare ili uweze kupata level halali ya oil
- Oil inayotumika kwenye injini kwa kawaida ni nambari 40
- Deef oil nambari 140
- Gear box ni oil nambari 90
· Mafuta ya Brake (Brake fluid) na clutch
· Maji ya betrii, yaani unafungua betrii na kuangalia kama
- Maji yamepungua unaongeza maji baridi Distrilled water
- Kama ni jipya umemwaga maji yote na kuweka Acid maarufu kama maji makali HCI
- Maji yakiisha ndani ya betrii , batrii itakufa baada ya hapo
- Unafunga tena bonet.
2. Sasa unaingia ndani ya gari na unaaangalia
· Kaa kwenye kiti chako na hakikisha kimekaa sawasawa
· Kagua pedle zote kama zinafanya kazi sawasawa yaani hapa tunazungumzia
- Brake kama iko sawa na inafanya kazi
- Clutch kama iko sawa na inafanya kazi
- Acceletator kama iko sawa na inafanya kazi.
· Kagua dashboard kama taa zote za vitu vyote zinafanya kazi vema yaani
- Water temperature gauge
- Alitanatory charge
- Oil gauge
- Fuel gauge
- Mail gauge .n.k.
· Waipa kama zinafanya kazi vema
· Hand brake kama inafanya kazi vema
· Usukani kama umekaa vema
· Mkanda
· Taa zite kama zinafanya kazi Hususani indicator
· Wema side mirror vema kukuwezesha kuona chochote kwa nyuma au pembeni
· Kioo cha kuangalia magari nyuma pia kiwekwe kukuwezesha kuona
Ukimaliza yote hayo sasa uko huru au salama kuendesha gari lako.
Great job
ReplyDeleteAsante saana cheif
ReplyDelete🙏🤓