WHEEL AND TYRE

Wheel ni nini ?
Huu ni muunganiko (combination) wa tire pamoja na rim.  Katika saizi mbalimbali zitokanazo na ukubwa na aina ya gari. (Size hizi zinaendana na radias- kipenyo cha kati)
          Tyre ni nini? 
Hii ni raba pana yenye umbo la duara ambayo inawekwa juu ya rim kwa kawaida raba hii inapoambatanishwa pamoja na rim tunapata kitu kimoja amabacho ni wheel (gurudumu)
Rim ni nini?
Hiki ni kifaa chenye umbo la mduaraambacho kimeundwa eidha kwa alminiumalloy au chuma (cast iron).
           Faida na kazi za wheel (gurudumu)
  1. Inafanikisha mwendo katika chombo husika, baada ya kukamilisha mzunguko wa gurudumu.
Hii inajieleza  yenyewe haihitaji uwe umeenda chuo cha VETA, fikiria kwamba unainjini yako , gear box , propeller, sheft, diferential alafu hauna magudumu je? Gari itajiongea kwenda uwelekeo wowote? Jibu ni hapana, hivyo gurudumu ni muhimu sana.
  1. Inabeba mzigo wote uliopo katika gari
Hapa tuelewe ya kwamba mzigo si mpaka uweke mafenesi na maaembe katika gari  lako ndio ukajua kwamba ndio mzigo hapana, bali kabla haujaweka kitu chochote ndani ya gari lako tayari kuna mizigo ambayo ni injini , gear box, body na chasesi hata pia vyote vina vyobebwa  hivyo , mzigo huo wote na ule utakaongeza wewe itabebwa na magurudumu .
Wewe toa sifa kuwa gari lako lina injini kubwa injini ina nguvu lakini kama magurudumu mabovu usijisifu kwakuwa bado hakuna usalama wa kukufikisha pale utakapo taka kwenda.
  • Yanasaidia katika kubadili uwelekeo
Magurudumu hususani ya mbele katika gari nyingi yana kazi ya kufanikisha utendaji kazi mzuri wa mfumo wa stering (steering system) katika kuongoza uwelekeo wa gari ikiwa hakuna uwelekeo wa gari.
  1. Yanasaidia dereva kuongoza gari wa urahisi.
Magurudumu (wheels) yanaweza kuwa sababu ya uendeshaji usiyo rahisi kwa dereva endapo hayapo katika viwango vinavyotakiwa hivyo magurudumu yaliyo mazuri yanampa dereva kuongoza gari.
Hapa ikiwa magurudumu hayako katika kiwango kinachofanana dereva atapata shida kuongoza gari kwani yaweza kuwa gari inavuta upande mmoja kitu amabacho ni usumbufu
Gurudumu la akiba (spare tire)

Hili ni gurudumu muhimu amabalo linatumika kwa dharura pale endapo moja kati ya magurudumu yako imepatwa na dhoruba .
Ni muhimu sana kutembea na gurudumu la akiba kwani kutembea katika gari lako bila gurudumu la akiba ni sawa na yule mtu ambae amevaa suruali au sketi nje lakini ndani hajavaa cochote ikitokea dharura hiyo suruari au sketi imechanika bila kutegemea anaadhirika.
Utalitambua vipi gurudumu la akiba
Gurudumu la akiba kwa kawaida linasifa zifuatazo kwanza linauwezo wa kuingia upepo mwingi sana kuliko umbo lake linavyoonekana, pia umbo lake huwa ni dogo mara nyingi rim yake huwa imeundwa kwa kutumia castiron, kusema hvyo sina maana kwamba gurudumu tofauti na hili haliwezi kuwa la akiba bali lengo hasa la kutengenezwa magurudumu ya aina hyo ni kwa ajili ya spair na kitaalamu inaitwaCOMPACT SPAIR TIRE.
Gurudumu la akiba halitakiwi kutumika kwa mda mrefu, tumia kwa mda mfupi ambapo unasogea tu kutoka ulipo kwenda kurepair au kubatili tire nyingine
            Faida za kubalansi magurudumu (wheel balancing)
Kubalansi magurudumuni kile kitendo cha kufanya usawa wa uzito wa ndani na ule wa nje katika gurudumu.
Faida ya kwanza magurudumu yako yataisha muda mrefu kwani ikiwa gurudumu ikiwa gurudumu haliko sawa katika uzito nwake wa ndani na ulewa nnje basi ni lazima tire itakula upande mmoja japokuwa kuna sababu tire kula upande mmoja.
Faida nyingine ni kuendesha kwa wepesi ,endapo uzito wa magurudumu yako hauko katika usawa inaweza kupelekea gari kuvuta upande japokuwa si kwa kiasi kikubwa hivyo ni jambo muhimu sana kwa yeyote anaependa gari lake.
              Angalizo
Usisubiri uone taili zako zinaisha upande mmoja au uendeshaji wa gari unakuwa mgumu kwa kuvuta upande mmoja ndio ujali kufanya balance ya magurudumu yako kwani kinga ni bora kuliko tiba (preventive maintanance is better than corrective maintenance).
        Aina za matairi
Kuna aina mbili za matairi ambazoni
  1. Radial tire
  2. Bias/cross tire
  • Radial tire
Hii ni aina ya tire ambayo muundo wake wa ndani unahusisha waya ngumu ambazo zimepanuliwa kwa mkato (crossing kwa kawaida ada hii ya tire inahusisha tabaka nne (four layer).
Mgawanyo wa matairi
Matairi pia yamegawanyika katika sehemu mbili nazo ni ;
  1. Tube tire
  2. Tubeless tire
Tube tire
Hii ni aina katika mgawanyo  matairi ambayo unatumia tube.
Tube ni raba laini ambayo ninawekwa kati ya rim na tire. Hizi tairi za tube mara nyingi huwa ni tairi za radial kwa sababu imeundwa katika tabaka tatu hivyo tube inaongeza na kuwa tabaka nne,  kusema hivyo si kwamba hakuna tairi za tube katika aina ya matairi ya bias
Tubeless tire
Hii ni aina katika mgawanyo wa matairi ambayo haitumii tube ndani yake.
Hii ni tairi ambayo inatumika sana kwa sasa kutokana na haina gharama kubwa katika matengenezo yake lakini pia matengenezo yake yanachukua muda mfupi ukilinganisha na zile tairi zenye tube ndani yake.
                  Ujazo wa upepo katika matairi (Tire inflation)
Kuna aina tatu za ujazo wa upepo katika matairi nazo ni:
  1. Proper inflation (ujazo sahihi)
Hii ni aina ya ujazo wa upepo katika matairi husika hivyo hii ni aina ya ujazo unaotakiwa kwa usalama.
Aina hii ya ujazo inalinda usalama  wa kwako mwenyewe lakini pia inalinda usalama wa tairi zako kwahivyo tairi zake zitaishi muda mrefu.
  1. Over inflation (ujazo kupita kiwango)
Hii ni aina ya ujazo wa upepo katika matiri amabyo upepo unaowekwa kwenye tairi unakuwa mwingi kupita kiwango elekezi kilichoainishwa katika tairi lenyewe.
                Hasara za over inflation
  1. Centre tire wear (tairi kulika katikati)
Aina hii ya ujazo wa matairi inasababisha tairi kuisha katikati.
  1. Kupasuka kwa tairi (tire bust)
Aina hii ya ujazo pia yaweza kusababisha tairi kupasuka ghafla na hatimae kusababisha ajali n akuleta hasara katika jamii zetu na taifa kwa ujamla
Tairi laweza kupasuka kutokana na kulika kati kwa tairi hilo au mzigo uliobebwa na gari hilo.
  • Under inflation (ujazo wa kiwango cha chini)
Hii ni aina ya ujazo wa matairi amabyo upepo unaojazwa unakuwa katika kiwango cha tairi ukilinganisha na kiwango tajwa au elekezi katika tairi lenyewe.
Hasara zitokanazo na under inflation
  1. Tire side wear (tairi kuisha upande)
Iwapo tairi imewekwa upepo katika ujazo wa chini tairi zitaisha katika pande mbili za tairi hilo kulia na kushoto bali katikati ya tairi hapataisha.
      2. Rim wear (kuharibika kwa rim)
Iwapo ujazo wa tairi ni mdogo unaweza kuathiri rim kwa kuipindisha na hata kuipasua unapofika katika matuta au mashimo barabarani.
Angalizo
Matairi yamekuwa ni chanzo kikubwa cha ajali za barabarani kutokana na kutozingatia hali ya matairi barabarani hayo hivyopnchukuwa hatuwa kuhusu tairi za gari lako leo pima ujazo wa upepo wa matairi yako kila unapotumia gari kwa kilometa 500.
             Sevisi ya matairi yako
Watu ni wengi wanaomoiliki  magari hata mafundi pia wanatambua sevisi ni kwa ajili ya injini na gear box, hapana si hivyo Evolution Garage leo inasema kwamba tairi nazo pia zinasevisi inayojitegemea kuondoa mawazo mgando kuanzia leo ya kufikiri sevisi ni katika injini pekee bali gari lote kwa ujumla linahitaji sevisi zikiwemo taili.
Wakati gani sevisi ya matairi inafanyika
Kitaalamu kuna vitu kinaitwa “tire rotation”
Hiki ni kile kitendo cha kubadilisha matairikutoka upande mmoja kwenda upande mwingine kwa kufuata aina ya gari na aina ya matairi (Radial au Bias tire)
Hii tire rotation inatakiwa kufanyika kila ifikapo kilometa 8000 ikiambatana na wheel balance pamoja na wheel alignment.
Kila unapofanya general sevisi ya gari lako ndani ya kilometa 3000 mpaka 5000 unapaswa pia kufanya wheel balance na wheel alignment.
Usisubiri mpaka gari iwe inavuta upande mmoja au tairi za mbele zinaisha upande mmoja ndipo ujali kufanya wheel balance au wheel alignment.
Tukifuata utaratibu huo hapo juu ni wazi kwamba tutakuwa salama sisi pamoja na magari yetu lakini pia matairi yatakuwa yakidumu Zaidi.

Comments

  1. Asante kwa maelezo mazuri na yaliyo Shiba.

    ReplyDelete
  2. Magurudumu yenye dama kubwa ni kweli huweza kuongeza ulaji wa mafuta wa gari yako?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

UMEME WA MAGARI

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI