MFUMO WA BREKI YA GARI

Huu ni mfumo miongoni mwa mifumo mbalimbali inayopatikana katika gari, Mfumo huu ni katika mifumo muhimu kiusalama katika gari
KAZI YA MFUMO WA BREKI
Mfumo wa breki hufanya kazi zifuatazo,
  • Kupunguza mwendo
  • Kusimamisha mwendo
AINA ZA BREKI
Kuna aina mbili za breki kama ifuatavyo
  • Mechanical Break
  • Hydraulic Break
  • Air Brake
MECHANICAL BRAKE
Hii ni aina ya breki ya kimakenikali ambayo inayegemea nguvu ya dereva tu katika utendaji kazi wake
Aina hii ya breki imekuwa ikitumika katika magari ya zamani lakini kwa sasa si rasmi
Picha ya mfumo huu ni kama unavyoona breki ya baiskeli. Kama hauna baisikeli nenda kaangalie hata baisikeli ya jirani ili ujue breki za mekamikali zinavyofanya kazi katika mfumo wake
VITU VINAVYOJUMLISHWA KATIKA MFUMO HUU
Pedali (Brake pedal)
Hiki ni kifaa kinachotumiwa na dereva kuvuta breki na kupsimamisha au kupunguza mwendo wa gari kwa wakati anapopaswa kufanya hivyo.
Springi Mrejesho (Return Spring)
Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kusaidia pedali kurudi nyuma baada ya kukanyagwa chini kwa lengo la kupunguza mwendo au kusimamisha gari
Waya mgumu wa kusafirisha nguvu.
Huu ni nwaya ambao mara nyingi huundwa kwa matirio ya alminiam alloy kwa kazi ya kusafirisha nguvu ya dereva mpaka kwenye matairi kuzuia mwendo kwa wakati unaotakiwa
Kigawanyishi cha nguvu (Junction Point)
Hii ni sehemu ambayo ile nguvu ya dereva inagawanywa kwenda upande wa kushoto na upande wa kulia. Kwa maana nyingine kwenda katika tairi la upande wa kulia na kushoto kwa tairi la upande kwa kilia kwa nguvu sawa na wakati mmoja
HASARA ZA KUTUMIA MFUMO HUU
Hasara moja wapo kuu ni kwamba inamchosha dereva kutokana na matumizi ya nguvu nyingi
Lakini pia haimpi dereva Amani , kwani kunauwezekano wa arm road tuchomoka ama kulegea na kufanya upatikanaji finyu wa breki
BREKI YA MAFUTA
Hii ninaina ya breki inayotumia mafuta katika utendaji kazi wake
JINSI INAVYOFANYA KAZI
Ufanyaji kazi wa mfumo huu unafanyika kwa mbadiliko wa nguvu ya mwanadamu (potential energy) kwenda kwenye mgandamizo (pressure energy) baada ya kutengenezwa nguvu ya mgandamizo inapelekea kuwa nguvu ya msukumo na hatimae kufikia lengo la kupunguza mwendo au kusimamaisha gari
VITU VINAVYOHUSISHWA KATIKA MSUKUMO HUU
Vifuatavyo ni vifaa mbalimbali vinavyohusishwa katika mfumo wa breki ya mafuta
  • Pedali
Kama nilivyokwisha kueleza kazi ya pedali katika mfumo uliopita wa mechanical brake, lakini kwa hapa tunaongeza kwa kusema ni kifaa kiunachotumika kusukuma nguvu ya mwanadamu kwenda katika masta silinda tutafamamu hapo mbele masta silinda ni nini?
  • Busta ya breki
Hiki ni kifaa kinachomsaidia dereva kusukuma pedali bila kutumia nguvu nyingi, hiki kifaa kimewekwa kati ya breki pedali na masta silinda, Ufanyaji kazi wake ni kwamba, Dereva anapo kanyaga pedali anazalisha hewa ambayo inaifanya pedali kuwa ngumu pasipo busta, lakini hii busta kazi yake ni kufyonza ile hewa kuivuta kwa kutumia nguvu ya injini na hewa hiyo inapelekwa kwenye matumizi ndani ya injini.
  • Masta silinda
Hiki ni kifaa kinachotumika kubadili nguvu ya ndereva kwenda kwenye nguvu ya mgandamizo (potenial energy into pressure energy)
Hapa ndipo pressure ya mafuta inapozalishwa Hiyo hiki ni kifaa muhimu kwani bila pressure hakuna breki kamwe
 
Bomba za mafuta
Bomba hizi hutumika kusafirisha mafuta yaliyo na mgandamizo kwenda katika matumizi kwa wakati, kwa kawaida kuna aina mbili za bomba hizi ambazo ni flexible piple yani bomba laini mpira na ring pipe yani ni ile bomba iliyoundwa kwa kutumia aluminum alloy
Wheel Cylinder
Hiki ni kifaa kinachotumika kubadili nguvu ya mgandamizo iliyozalishwa kutoka kwenya master silinda na kuwa nguvu ya msukumo na moja kwa moja nguvu hii iyasukuma Brake pad ama brake shoe na hatimae kupata breki
Brake Pads na Brake Shoe
Hiki ni kafaa kinacho maliza ama kukamilisg adhna ya dereva katika kupunguza mwendo ama kusimamaisha mwendo kwani kifaa hiki nkinaposukuma kwa nguvu ya msukumo kinagusana mija kwa moja na rotor ama drum na hatimae kuleta ukinzani wa mwendo.
Kwa kawaida matirio yanayotumika kutengeneza prake pads ana brake shoe yanaitwa ASBESTOS MATERIAL haya ni material mepesi yenye uwezo wa kukabiliana na msuguano bilaKuathiri rotor wala drum

AIR BRAKE
Hii ni aina ya breki ambayo utendaji kazi wake unategemea hewa]
VITU VINAVYOHUSISHWA KATIKA MFUMO HUU
Tutataja vitu vichache ambavyo havikuwepo kwenye aina mbili zilizopita
AIR COMPRESSOR
Hiki ni kifaa ambacho kinazalisha upepo ambao unatumika kukamilisha utendaji kazi wa mfumo huu
BUSTA
Hiki kifaa ni tofauti na kili kilichotajwa hapo awali, Kwani kile cha mawanzo kipo katikati ya pedali na masta silinda, Hiki kinapatikana katika kila tairi yaani la mbele na nyuma katika kila upande
Katika mfumo huu upepo ndio nunaotoa nguvu ya msukumo kusukuma brake shoe na brake pads
MGAWANYIKO WA BREKI
Breki zimegawanyika katika sehemu mbili amabzo ni
  • Rotor brake
  • Drum brake
ROTOR BRAKE
Hizi ni breki ambazo zinatumia kifaa chenye muundo wa ngoma na katika brake za aina hii zinatumia brake pads
DRUM BRAKE
Hizi ni brake ambazo zinatumia kifaa chenye muundo wa ngoma na katika brake za aina hii zinatumia brake shoe.
NB:
Tambua ya kwamba kuna gari zinatumia drum mbele na nyuma na kuna gari zinatumia rotor mbele na nyuma lakini pia kuna gari zinatumia rotor kwa upande wa mbele na nyuma.
HAND BRAKE
Hii ni brake ambayo inatumia kuegesha gari kwa usalama Zaidi unapopaki gari.
MATATIZO YANAYOTOKEA KATIKA MFUMO WA BREKI
Hili ni moja kati ya matatizo yanayotokea katika mfumo wa breki. Tatizo hili linasababishwa na vitu vikubwa viwili ambavyo ni mfumo kuingiwa na upepo ama spring ya mrjesho kuharibika lakini pia inaweza kuchangiwa na masta silinda inayozalisha kidogo pia yaweza kufanya pedeli kunasia chini
Pedeli kushuka Zaidi baada ya kukanyaga
Hili nalo pia ni tatuzo kwasababu linaweza kupelekea breki kupotea kidogo kidogo
Sababu za tatizo hili ni upepo katika mfumo kwani baada ya kukanyaga mafuta yataendelea kutembea kidogo kidogo sehemu zilizo wazi maana zilizo na upepo
Lakini pia tatizo hilo linaweza kusababishwa na kuvuja kwa mafuta katika sehemu yoyote ile, iwe katika bomba la mafuta, masta silinda au wheel silinda
Pedeli kuwa ngumu kupita kiasi
Kitendo cha pedeli kuwa ngumu Zaidi inapokuwa juu kwani itahitaji nguvu Zaidi ya dereva ambapo haipaswi kuwa hivyo
Tatizo hili linasababishwa na busta kuwa haifanyi kazi kabisa au kufanya kazi kwa kiwango kidogo, Kwni hapo awali tulisema kwamba busta kazi yake ni kumsaidia dererva kuvuta pedeli ili asitumie nguvu nyingi

Lakini pia tatito hili linasababishwa na piston zilizopo ndani ya masta silinda ama wheel silinda kunasa na nkushindwa kutembea
Breki kupatikana kwa kiasi kidogo
Kupatikana kwa breki kwa kiwang kidogo katika gari, hilo ni tatizo ambalo linaweza kuharatisha maisha ya dereva lakini pia usalama wa chombo chenyewe kwani yaweza kutokea kitu cha ghafla wakati unaendesha ambacho ungeweza kukiepuka kama ungekuwa nabreki zilizo sahihi
Tatizo hili linasababishwa na kuisha kwa brake pads ama brake shoe hivyo inashindwa kubana vizuri katika rotor ama katika drum hivyo bado mwendo unaendelea ila kasi yake inapungua hivyo kama unaelekea kugonga mti ni lazima utagonga kwani hutoweza kusimama kwa haraka
Lakini pia tatizo hili linaweza kusababishwa na upepo katika mfumo wa mafuta kidigo katika tank la mafuta aya breki
Pedali ama gari kutetemeka unapokanyaga breki
Hili ni tatizo kwani dereva na wote waliopo kwenye fari hautakiwi kusumbuliwa na gari bali unatakiwa kuwa katika hali ya kustarehe ndio maana halisi ya kubuniwa kwa mfumo wa mneso katika gari ili kufanya mtumiaji wa gari kuwa katika hali nzuri wakati wote. Hivyo endapo unakanyaga breki na gari inatetemeka hiyo ni karaha na kukosa Amani kwa mtumianj maan inapelekea kupotea Amani ya usalama
Lakini pia tatizo hili linaweza kusababishwa na uchafu na kutofanya kazi kwa ABS kwa magari amabyo yanatumia mfumo huo hususani magari ya kisasa,
NB:
ABS ni mfumo mpya ambao unatumika sana katika magari ya kileo mfumo huu unahusisha kifaa ambacho kinagawa mafuta katika miguu yote mine baada ya kusukumwa kwa mgandamizo kutoka katika masta silinda
Hicho kifaa kinafanya kazi yas kugawa mafuta ya breki kinatambulika kama ABS Box kwa maan ya automatic brake system na kina kiashiria cha tatizo litakalo jitokeza katika mfumo, hivyo ni kifaa muhimu sana kwa madereva
NJIA ZA KUEEPUKA MATATIZO KATIKA BREKI ZA GARI LAKO
Hakikisha mafuta yapo katika kiwango kinachofaa
Kwa kawaida tanki la mafuta ina viashiria ya viwango vya mafuta vilivyomo ndani yake ambavyo ni low na full au high, Hivyo hakikisha mafuta yapo katika mshale wa Full/High usizidishe Zaidi ya hapo wala usipungue chini ya hapo
Kufanya ukaguzi wa brake pads and shoe
Kila baada aya kilometa 3000 unapaswa kukagua mfumo wako wa breki katika gari na kama pads ana shoe zime kwisha usikubali kuziacha ili kuepukana na adhali zitakazo weza kijitokeza kama ilivyoelezwa hapo juu zitokanazo na kuisha kwa brake pads ama shoe
Kubadili ama reface rotor kama ifuatavyo
Iwapo diski rotor imechimbika kwa kiasi kidogo inafgaa ku reface (kuchonga) lakini kama imechimbika sana na imekwisha ilio ulifurahie gari lako unapolitumia na usalama wa uhakika
Muone mtaalamu unapoona tofauti
Punde tu unapoona tofauti yoyote katika breki yako muone mtaalamu kwani unaweza kuzarau kumbe tatizo ni kubwa na litapelekea adhali kubwa Zaidi kwako mwenyewe na kwa jamii hivyo kufabya hivyo ni busara Zaidi
USHAURI
Endesha mwendo wa utaratibu yaanimwendo wa kawaida na katika speed ishirini mpaka thelathini kama hakuna sababu ya lazima ya kufanya utembee Zaidi ya spidi hizo. Kwani usijiaini kwa kutegemea breki yaweza kutokea tatizo la kiufundi ghafla katika mfumo wa breki na kushindwa kijitetea
Under #evolution 
Toa maoni yako hapo chini asante. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

UMEME WA MAGARI

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI