JINSI YA KU ROOT SIMU YAKO YA SMARTPHONE (ANDROID)
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika Mawasiliano, Kuhifadh i kumbukumbu za muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program ambazo huwekwa kwenye mfumo wa simu (Operating System). Programu hizo hubeba maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji kufanyia mambo mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti), Calculator, nk. Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji wa Simu au Computer ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi yake. Katika miongo michache iliopita zimetengenezwa program nyingi mpya na zenye maboresho makubwa na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika program mbalimbali unaleta ukuaji katika Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia zimeleta urahisi na ufanisi. Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatif...