JINSI YA KUJIFUNZ UDEREVA

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA

WA MAGARI

SEASON 1


VIPENGELE VYA UDEREVA VYA KUJIHAMI.
Ili kutekeleza kanuni ya kuzuia ajali, Dereva yeyote anatakiwa kuelewa vizuri mambo ya msingi yafuatayo;-

1.       Kujua
2.       Kuwa macho
3.       Kuangalia mbele
4.       Kuamua
5.       Ujuzi wa kugundua , hatari kwa haraka

KUJUA

Dereva anapaswa kuelewa michoro na alama za barabarani.
i.                     Alama za barabarani na michoro inawakilisha lugha, ambayo kila mtumiaji wa barabara anatakiwa kuijua vizuri, kuiheshimu na kuitafasiri kama inavyotakiwa.
ii.                   Kwa bahati nzuri inawakilishwa na vbitambulisho vya vikundi vikuu vitatu
a.       Rangi Nyekundu, Nyeusi, uhNjano, Nyeupe, bluu, kijani.
b.      Umbile Mviringo, Pembe tatu, Pembe nne na pembe tano.
c.       Alama – Maandishi, Picha na Michoro.
iii.                  Alama na michoro ya barabarani ni lazima ziwe na sifa zifuatazo.
a.       Zilenge kuongeza ufanisi wa mtandao wa barabara.
b.      Zitoe ujumbe ambao ni wazi unaoeleweka kirahisi kwa kila mtumiaji wa Barabara.
c.       Zizingatie sheria za  usalama barabarani za kitaifa na kimataifa
d.      Ziwe na muundo wa alama moja kitaifa unaolingana na makubaliano ya umoja wa kimataifa kwa alama za msingi.
e.      Ziwekwe sehemu ambazo ni lazima kuwepo, ili zitoe ujumbe sahii kwa watumia Barabara,
f.        Ziwekwe umbali unaotakiwa kutoka sehemu husika
g.       Zifanyiwe matengenezo ya marakwa mara.

Mambo ya msingi ya kujiuliza kwanza
a.       Alama ni kiashirio kinachomuongoza mtu kwenye mambo na kumfanya afanye mambo vizuri.
b.      Alama za barabara ni uongozi uliowekwa kisheria  kutoa muongozo wa kisheria  ili kumuwezesha dereva  aweze kufanya kazi zake kirahisi na  kwa ufanisi  ili kwamba atumiapo barabara  aweze kwenda kwa uysalama zaidi bila kupata au kusababisha ajali.
c.       Alama za barabarani ni kitu ambacho hakitarajiwi kutokuweko
d.      Wataalamu waliamua kukaa na kutunga alama za usalama barabarani  alama hizo zimegawanyika katika makundi makuu matano
·         Alama za Amri
·         Alama za Onyo
·         Alama za taarifa
·         Alama za maelekezo
·         Alama za michoro chini ya barabara , taa za kuongoza watumiaji wa barabara.

Alama za Amri
Alama hizi zimegawanyika katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
-          Amri za kukataza.
-          Amri za kulazimisha au kuruhusu.
-          Amriza kutoa kipaumbele

Amri za kukataza ;-
Alama hizi zina waonyesha watumiaji wa barabara sehenu ya barabara iliyokatazwa au mwisho wa sehemu iliyokatazwa  kufanya jambo Fulani  kama itakavyoonyeshwa  kwenye alama yenyewe alama hizi ni halali

·         Katika mwelekeo wa kawaida wa wanaotumia barabara
·         Kutoka sehemu iliyopo hadi njia panda iliyo karibu na alama husika .
Alama za amri ya kukataza zina umbo la mviringo, mpaka mwekundu na picha au mchoro wenye rangi nyeusi, nyekundu au bluu katika madhari
Alama au amri ya kukataza zinawekwa karibu sana na sehemu husika 

Alama za kulazimisha  au kuruhusu
Ø  Hizi ni alma zinazzotumika kwa watumia barabara  kuelekea mwelekeo au njia Fulani kati ya nyingi zilizopo kwenye  njia panda , pia alama hizi zinatumika kuwaongoza wanaotembea kwa miguu na wapanda baiskeli kwenye njia moja kati ya njia zilizopo kwenye eneo husika
Ø  Amriza kulazimisha zina umbo la mviringo mpaka mdogo mweupe na picha ai mchoro mweupe katika madhari nyuma bluu alama hizi zinawekwa karibu sana na njia panda
Ø  Alama za kipaumbele na kupisha njia panda ni sehemu yenye migogoro mingi kati ya watumia barabara kuliko sehemu nyingine yoyote ile barabarani. Ili kurekebisha migogoro hiyo kati ya watumia barabara. Sheria ya Usalama barabarani  inatumika (toa kipaumbele  kwa madereva wa magari wanaokaribia njia panda kutoka kulia ) lakini sehemu yenye magari mengi  ambapo madereva hawawezi kutathimini vizuri hatari iliyopo basi sehemu hiyo njia panda sheria ya usalama barabarani haitatumika  tena badala yake zitatumika alama za kipaumbele
Ø  Alama hizi zina maumbo mbali mbali kulingana na ujumbe au amri inayokusudiwa katika alama husika.

Alama za tahadhari au Onyo
Ø  Alama hizi zinawaonya madereva na watumia barabara wengine juu yaq hatari iliyopo au inayoweza kuwepo mbele yao
Ø  Alama hizi zinawqekwa upande wa kushoto wa barabara  kati ya mita mia hadi  mia mbili (100-200m) toka sehemu yenye hatari
Ø  Sehemu zenye njia panda nyingi hasa mjini umbali huo hupungua hadi mita hamisini  (50m)
Ø  Sehemu ya barabara yenye alama hizi dereva anatakiwa kupunguza kasi ya gari lake.
Ø  Alama za tahadhariu au onyo zina umbo la pembe tatu lenye kitako pembe mbili chini, mpaka mwekundu na picha au mchoro wa hatari iliyopo au inayoweza kutokea mbele katika mandhari ya nyuma nyeupe.

Alama za Taarifa
Ø  Alama za taarifa huwataarifu madereva na watrumia barabra wengine juu ya barabara , sehemu muhimu na sehemu senye huduma mbalimbali ambazo ni muhimu kwao , kati ya alama hiziz zipo pia  zenye uhusiano na sheria ya usalama barabarani ambazo zinatoa masharti Fulani ambayo  mtumiaji wa barabara akiamua kutumia sharti afuate sheria  na si vinginevyo Kwa Tanzania ni hiari ya dereva kutumia barabara hiyo ,lakini akiamua ni lazima aendeshe gari lake uelekeo ulioonyeshwa kwenye alama hiyo.
Ø  Alama za maeneo ya huduma, hizi ni taa ni alama zinazowafahamisha madereva na watumia barabara wengine juu ya huduma mbalimbali wanazoeweza kupata katika maeneo husika
Ø  Alama hizi zina umbo la pembe mraba nne, ulingo wa Bluu picha nyausi au nyekundu katika madhari nyeupe nyuma 

Alama za maelekezo
Ø  Hizi ni alama za kuwafahamisha madereva wa magari sehemu maalumu nba muhimu
Ø  Alama hizi zina umbo la pembe nne Mstatili au mraba ulingo wa bluu picha nyeupe au nyeusi madharri ya bluu au kijani nyuma.
Ø  Alama hizi zinawekwa kabla ya njia panda  au kwenye njia panda  ili kuwasaidia madereva na watumiaji wengine wa barabara  kuchagua barabara  zinazofaa kuwafikisha waendako na kuwaongoza kwenye mtanadao wa barabara kupita na hata kuzunguka  kwenye maeneo ya makazi ya watu

Alama za michoro ya chini ya barabara na taa za barabarani
Ø  Michoro ya barabarani ni ni mmichoro iliyochorwa kwa  lengo la kurekebisha msongamano wa magari pamoja na kuwaonya au kuwaongoza watumiaji wa barabara
Ø  Michoro hiyo ya barabarani imegawanyika katika makundi makuu yafuatayo;-
*      Mistari ya Onyo
*      Mistari ya kukataza
*      Mistari inayogawa njia katikati ya barabara  ya magari
*      Mistari inayogawa barabara
*      Mistari inayogawa njia ya magari ya abiria  katika barabara
*      Mistari ya kutokea  pembeni mwa barabara  ya magari
*      Mistari ya kipaumbele
*      Mistari ya kusimama
*      Mistari hii pia huchoirwa karibiu na njia panda  sehemu ya barabara hii dereva hatakiwi kuvuka njia kwa sababu ya hatari iliyopo ikiwa atavuka basi avuke kwa tahadhari kubwa
Taa za kuongoza watumia barabara
Ø  Taa hizi zinalenga  kuondoa migogoro kati ya watumia barabara  kwenye njia panda au barabara zenye matumizi makubwa
Ø  Taa nyekundu humaanisha usiingie njia panda simama
Ø  Nyekundu na njano usiiingie nja panda simama
Ø  Njano usiingie kwenye njia poanda simama
Ø  Kijani ingia kwenye njia panda endapo ni salama.

Comments

Popular posts from this blog

UMEME WA MAGARI

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI