PROGRAM TANO(5) ZINAZOWEZA KURUDISHA SMARTPHONE ILIYOPOTEA

PROGRAM TANO(5) ZINAZOWEZA 
KURUDISHA SMARTPHONE ILIYOPOTEA

1. LOOKOUT. Hii ni moja ya programm inayomwezesha mmliki wa simu aina ya android kubaini mienendo ya simu iliyopotea. Huku ikitoa taarifa  mahala simu ilipo , Pia hii programu inapiga picha za siri bila mwizi au aliyechukua kutambua na kutuma moja kwa moja  kwa  anuani yako uliojisajilia katika hiyo programm.Ina uwezo wa kufunga ama kufuta habari binafsi zilizondani ya simu na endappo upo karibu na mtu mwenye simu yako programm inakuwezesha  kuruhusu simu itoe alarm na kumkamata mwizi.

2. LOOKOUT PLAN B. Tofauti ya programm hii na ya kwanza ni kuwa Lookout plan B hutumika na baadhi ya simu tu zinazotumia mifumo ya android. Na wakati programm zote katika hii list zinahitaji kuwekwa katika simu kabla haijaibiwa, Lookout plan b inaweza kuingizwa katika kifaa kilichopotea ama kuibiwa hata baada ya mwizi kutokomea Ni kwa njia ya mtandao Lookout Plan B huweza kufikia simu iliyopokonywa.


3. PREY. Kama zilivyo programm nyingine hii pia inapatikana Google play , yaani katika simu zitumiazo android . Au kwa urahisi sana zinajulikana kwa jina la '' simu za tachi' '(touch). Prey ni programm ambayo inauwezo wa kuonyesha mitandoo yote inayotumiwa na simu yako iliyopotea. Lakini hata kama kulikuwa na picha za muhimu hii ni prograam iayoweza kuzihifadhi katika account au anuani yako ya google.Zaid Prey huweza kutumika hata kutafta laptop na tablets zilizopotea.

4. FIND MY PHONE. Hii programm inatofautiana na nyingine kwa kuwa inawafaa watumiaji wa Iphone na vifaa vingine vinavyotengenezwa na  kampuni  ya Mac.Ambao ni wazalishaji wa ipod, ipad na simu zaIphone.  Habari nyeti za mtu alizoacha katika simu hupelekwa na  progrmm hii hadi uwanja wa icloud. ambako mmliki wa simu hufika kwa kufanya usajili mdogo. Hapa utajua simu yako iko wapi, nani anaitumia kwa kutazama picha zilizopigwa kwa usiri wakati mwizi akiitumia.                                            

5. ANDROID DEVICE MANAGER, Ni aina nzuri ya programm katika kurudisha simu kwa kuwa ina sifa kama programm nyingine ikiwemo ile ya kuwafaa watumiaji wa android, Pia ina mambo muhimu ya kuzingatia kama ; kupata simu iliyopotea .kwanza. inatakiwa iwe imeunganishwa na mtandao, pili,  iunganishwe na na programm hii kabla haijaibiwa,  tatu, simu itaonekana baada ya kuwa karibu na minara ya simu, huduma za wireless, bloothooth na mifumo mingine yenye kutuma mawasiliano katika satellite za google , nne, kuifikia simu iliyopotea unatakiwa kutumia simu tofauti, computer au kifaa kingine. Mwisho hii programm kama hizo zilizotajwa juu hupata simu ikiwa imewashwa na sio kuzimwa






Comments

Popular posts from this blog

UMEME WA MAGARI

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI