SOMO JUU YA MAANA YA “CHIP” KWENYE KOMPYUTA

“Chip” ni kipande kidogo kinachofanya muunganiko wa sehemu mbalimbali za Kompyuta ambacho kimezungukwa/kimeundwa na Saketi mbalimbali, Kipande hiki mar azote ki[po kwenye mfumo wa “Silcon”. Chip ziko na ukubwa chini ya inchi moja ya mraba. Chip imezungukwa na maelfu ya “transistor” za kielectronic.  “Chip” hizo zimejishiza kwenye Ubao Mama (Motherboard/printed circuit boards),uwepo wa Chip hizo husaidia sana Kuendesha mfumo mzima wa Kompyuta kwa ujumla.
“Chip”ndiyo imebeba mfumo mzima wa umeme kwenye Kompyuta, hapa tunazungumzia pia  uwepo wa “processor” au “graphics chip”.

Katika Dunia hii zipo kampuni mbalimbali ambazo zinatenegeza “chip” mbalimbali ambazo ni kama ifuatavyo;
-Intel 48.7, Samsung 28.6, TI 14, Toshiba 12.7, Renesas 10.6, Qualcomm 10.2, ST 9.7, Hynix 9.3, MicBroadcom 7.2, Broadcom 7.2

Zipo “chip” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa Ubao mama kwenye Kompyuta.
1. RAM
RAM ni kichocheo muhimu sana katika utendaji mzima wa Kompyuta, mara nyingi hufanya kazi kama kibarua kwenye mfumo wa utendaji wa vifaa vitatu vinavyotegemeana hapa nina maana ya RAM ” yenyewe, “Processor” pamoja na “Hard Disk”. RAM nayo inaangukia kwenye aina za Chip zinazounda mfumo mzima wa Kompyuta.
2. Microprocessor- Hapa tunazungumzia kwa kifupi kuhusu CPU, Hii hujulikana kwa kiwango kikubwa kama ubongo unaounda mfumo mzima wa Kompyuta,   Cpu nayo ipo kwenye mfumo huo huo wa chip, kwa kawaida Cup huundwa na arithmetic logic units (ALUs) ambayo imepachikwa kwenye “large-scale integration (LSI)”, sehemu hii huundwa na maelfu ya “transistor” zinazojishikiza kwenye sehemu hiyo ya “LSI”.
3. Zipo pia chip mbalimbali zinazowezesha kamera kufanya kazi, kuendesha mfumo mzima wa “applications” kwenye Kompyuta, kusaidia kuendesha mfumo wa modem kwenye Kompyuta hizi zote ni chip zinazosaidiaana kila sehemu ili kuunda mfumo mzima wa utendaji kwenye Kompyuta.
        
Muundo wa “Chip”.
Chip ziko kwenye mfumo wa aina tatu ambazo hujumuisha;
1. Njia moja (single in-line packages (SIPs), hii hujumuisha chip yenye mguu mmoja na pin zimejipanga mfulilulizo kwenye mraba.
2. Njia  Mbili (dual in-line packages (DIPs), hii huwa na miguu Zaidi ya nane hadi 40 na hujipanga kwenye safu mbili za kwenye Saketi moja.
MATATIZO YANAYOZIKUMBA “CHIP” KWENYE KOMPYUTA.
Kwa kuwa Chip hizi kila iitwapo leo pale unapokuwa unatumia Kompyuta huweza kupata hitilafu na hata kupelekea kufa/kuharibika kwa chip hizo. Mambo/ matatizo yanayosababisha chip kuharibika ni pamoja na.
1. Uchafu/vumbi kwenye Kompyuta, hii hutokea pale ambapo unakuta mtu anatumia Kompyuta bila kufanya usafi, ambapo kutu huganda kwenye chip na hata kupelekea kuharibika kabisa.
2. Kuongezeka kwa joto (temperature) kwenye Kompyuta,
3. Kuishi kwa muda mrefu kwa chip, hupelekea pia kushindwa kufanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu na hata kupelekea kufa kabisa, hivyo suluhisho lake ni kumpata fundi kwenye uelewa wa kuweza kugundua chip yenye matatizo na kuibadilisha.
Kwa kumalizia ni kwamba kuharibika kwa chip hupelekea kuharibika na sehemu mojawapo ambapo chip hiyo inakuwa inaendesha sehemu hiyo, mfano, hapa kama chip inaendesha mfumo wa kusababisha kioo kuwaka pale inapopata hitilafu hupelekea kioo kushindwa kuwaka kabisa.

N.B. Kumekuwa na utaratibu wa watumiaji anapoona Kompyuta yake haiwaki anakimbilia kununua Ubao Mama(Motherboard), wa Kompyuta bila kupima kwa kina na kufanya uchunguzi wa hali ya juu ili kupata tatizo au chip ambayo inasumbua. Hivyo upatapo tatizo hilo nenda kwa “Technician” mwenye ujuzi wa hali ya juu aifungue Kompyuta yako na kuipima kwa weredi ili kugundua ni wapi Kompyuta yako ina hitilafu.

Tunakaribisha maoni,ushauri, (Comment, Like, shares) maana sote tunatamani kujifunza Zaidi ili jamii yetu iwe na uelewa Zaidi juu ya Matumizi ya Kompyuta kwa ujumla.
Karibu sana CATAUX COMPUTERS, uwapo na Tatizo lolote kwenye Kompyuta yako, USISTE kututafuta ili kutatua tatizo lako hilo.

Tupo DAR, MWENGE STAND YA ZAMANI.
Mawasilaiano  : 0714003752
                        : 0682566622

Comments

Popular posts from this blog

UMEME WA MAGARI

Mfumo wa Upoozaji Engine ya Gari. (Car Cooling System)

JINSI YA KUJIFUNZA UDEREVA WA MAGARI